WAZIRI MKUU: RCs, DCs NENDENI MKAGUE MASOKO, MADUKA KUPATA BEI HALISI ZA BIDHAA

*Awataka pia wahamasishe wananchi kuhusu Sensa ya Makazi na Watu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wafanye ziara kwenye masoko na maduka ili kupata hali halisi ya bei za bidhaa na wachukue hatua kudhibiti upandaji holela wa bei hizo.  Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Ijumaa, Aprili 22, 2022)